

Lugha Nyingine
港媒称习近平肯定林郑月娥治港工作}
Washiriki wa Shindano la Kanda ya Afrika la Mashindano ya Kimataifa ya Uvumbuzi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ya China wakiwasiliana jijini Nairobi, Kenya, Julai 25, 2025. (Xinhua/Yang Guang)
NAIROBI - Lavenda Chepkirui, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 25 kutoka Chuo Kikuu cha Kabianga nchini Kenya, amepiga hatua karibu zaidi kufikia matumaini yake ya kukifanyia mageuzi kilimo barani Afrika kwa ufumbuzi rafiki kwa mazingira.
Uvumbuzi wake – vitu vya kufunika udongo vinavyoweza kuoza vilivyotengenezwa kutokana na uchafu wa mazao – umempa ushindi wa medali ya dhahabu katika Shindano la kwanza la Kanda ya Afrika la Mashindano ya Kimataifa ya Uvumbuzi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ya China 2025, ambalo limehitimishwa Ijumaa jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
"Kwa kutumia vitu vinavyoweza kuoza vya kufunika udongo, wakulima wanaweza kuongeza mavuno yao kwa kuondoa magugu na kuhifadhi unyevu," Chepkirui ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye hafla hiyo ya utoaji tuzo.
Chepkirui ni miongoni mwa wanafunzi 559 kutoka vyuo vikuu 115 vya Afrika waliowasilisha jumla ya miradi 185 ya uvumbuzi kwenye shindano hilo, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Nanjing (NAU) cha China. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanya shindano la kikanda katika bara la Afrika.
Picha hii iliyopigwa Julai 25, 2025, ikionyesha ukumbi kwa ajili ya hafla ya kufunga Shindano la Kanda ya Afrika la Mashindano ya Kimataifa ya Uvumbuzi ya Wanafunzi wa Vyuo ya China mjini Nairobi, Kenya. (Str/Xinhua)
Miradi ya uvumbuzi kwenye shindano hilo yalihusisha nyanja mbalimbali kutoka teknolojia za kilimo na chakula hadi AI na uendelevu wa mazingira. Baada ya tathmini za kitaalamu, timu 30 kutoka vyuo vikuu 21 katika nchi tisa za Afrika zilipokea tuzo katika vipengele mbalimbali.
Chepkirui amesema jukwaa hilo si tu lilimruhusu kuonyesha wazo lake bali pia limetoa ushauri muhimu.
Roselida Owuor, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Utafiti wa Kisayansi na Uvumbuzi ya Serikali ya Kenya, amesema shindano hilo linatumika kama njia ya uzinduzi kwa vijana wa Afrika kuanzisha na kuendeleza ufumbuzi wa kienyeji kwa changamoto za bara.
"Kenya ina nia ya kulea vijana kuufanya uvumbuzi wao kuwa biashara kupitia kuanzishwa kwa vituo vya uvumbuzi kote nchini," amesema Owuor.
Zhu Yan, makamu mkuu wa NAU, amesema shindano hilo si tu ni jukwaa la vijana wa China na Afrika kuonyesha hekima yao ya uvumbuzi lakini pia ni mfano wa utekelezaji wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na kuimarisha ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Kiplangat Felix, mshiriki wa Shindano la Kanda ya Afrika la Mashindano ya Kimataifa ya Uvumbuzi ya Wanafunzi wa Vyuo ya China akifanya uwasilishaji mradi mjini Nairobi, Kenya, Julai 25, 2025. (Str/Xinhua)
Simulizi nyuma ya miradi iliyoshinda pia zinaangazia jinsi uvumbuzi, mawasiliano ya kitamaduni, na utatuzi matatizo kwa vitendo vinavyokusanyika ili kukidhi mahitaji ya Afrika yanayobadilika.
Silvia Christopher Mganga, Mtanzania mwenye umri wa miaka 27 mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Egerton, alikuwa mmoja wa timu iliyoshinda medali ya dhahabu ambayo ilianzisha mradi wa kupandikiza nyanya.
Msukumo wake ulitokana na kuwatazama wazazi wake wakihangaika na upotevu wa mazao kama wakulima wadogo wa nyanya.
"Mradi wetu unachanganya miche ya mizizi ya Kichina na aina za nyanya za kienyeji, ikitengeneza mazao ambayo ni sugu kwa magonjwa na yenye mavuno mengi," Mganga amesema.
Adams Abdul Hamid, mshiriki wa Shindano la Kanda ya Afrika la Mashindano ya Kimataifa ya Uvumbuzi ya Wanafunzi wa Vyuo ya China akifanya uwasilishaji mradi mjini Nairobi, Kenya, Julai 25, 2025. (Str/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma